Back

ⓘ Augusto wa Bourges
                                     

ⓘ Augusto wa Bourges

Augusto wa Bourges alikuwa mlemavu wa mikono na miguu aliyetumia sadaka aliyopewa makao ya upwekeni kwa heshima ya Mt. Martino.

Alipomaliza tu, alipona kikamilifu ulemavu wake akakusanya wamonaki akawa padri na abati akidumu katika sala.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Oktoba.