Back

ⓘ Ambrosi Edwadi Barlow
Ambrosi Edwadi Barlow
                                     

ⓘ Ambrosi Edwadi Barlow

Ambrosi Edwadi Barlow, O.S.B. alikuwa Mkristo wa Kanisa la Anglikana kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki mwaka 1607.

Baada ya kuhamia Ufaransa, aliingia seminari kwa kengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali. Baadaye alijiunga na monasteri ya Wabenedikto 1615 na kupewa daraja ya upadri 1617.

Hapo alirudi Uingereza alipofanya uchungaji kwa siri kwa miaka 24 katika eneo la Lancaster na alikataa kukimbia hata baada ya mwili wake kupooza na dhuluma ya mfalme Charles I kutisha zaidi. Hivyo alikamatwa na kuuawa kikatili sana

Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 15 Desemba 1929, halafu Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39.

Sikukuu yake ni tarehe 10 Septemba.

                                     

1. Marejeo

 • Moss, Fletcher 1903 Pilgrimages to Old Homes. Didsbury
 • Camm, Bede 1931 Nine Martyr Monks
 • Allanson, Biographical MSS. preserved at Ampleforth Abbey: MS. I
 • Challoner, Richard; John Hungerford Pollen, ed. 1924 Memoirs of Missionary Priests
 • Gillow, Joseph 1885 Bibliographical Dictionary of English Catholics. London
 • Dodd, Charles 1739 Church History of England. Brussels
 • Rhodes, W. E. ed. 1909 The Apostolical Life of Ambrose Barlow. Manchester: Chetham Society
 • Moss, Fletcher 1891 Didsbury. Manchester
 • Moss, Fletcher 1894 Chronicles of Cheadle, Cheshire. Didsbury
 • Butler, Alban 2000 Lives of the Saints, vol. 9 revised ed.
 • New Catholic Encyclopedia 1967