Back

ⓘ Arsasi wa Nikomedia
                                     

ⓘ Arsasi wa Nikomedia

Arsasi wa Nikomedia alikuwa askari wa Dola la Roma mwenye asili ya Persia.

Baada ya kuungama hadharani imani ya Kikristo wakati wa kaisari Licinius, aliacha jeshi aende kuishi upwekeni karibu na Nikomedia.

Alihimiza wakazi wa mji huo kusali na kufanya toba akitabiri tetemeko la ardhi lililouangamiza pamoja na kumuua mwenyewe.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Agosti.