Back

ⓘ Papa Klementi I
Papa Klementi I
                                     

ⓘ Papa Klementi I

Papa Klementi I alikuwa Papa kuanzia takriban 92 hadi kifodini chake takriban 99.

Alimfuata Papa Anacletus akafuatwa na Papa Evaristus.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 23 Novemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 24 Novemba au 25 Novemba upande wa mashariki.

                                     

1. Sala yake

Wewe umefunua macho ya mioyo yetu, ili tukujue wewe Mungu pekee, uliye juu sana katika mbingu za juu, mtakatifu unayekaa kati ya watakatifu, ambaye unanyenyekeza ufidhuli wao wenye kiburi, unabatilisha mashauri ya mataifa, unawainua juu wanyonge na kuwashusha wanaojikweza, wewe ambaye unatajirisha na kufukarisha, unaua na kuhuisha, ambaye peke yako unafadhili roho na ni Mungu pekee wa kila mwenye mwili, unatazama vilindi, unachunguza matendo ya wanadamu, unawasaidia waliopo hatarini na ni mkombozi wa waliokata tamaa, ni muumbaji na mtunzaji wa roho zote, unazidisha mataifa duniani, ambaye kati ya wote umewachagua wanaokupenda, kwa njia ya Yesu Kristo Mwanao mpendwa, ambaye kwa njia yake umetulea, umetutakasa na kutuvika heshima.

Tunakusihi, Bwana, uwe kwetu msaidizi na tegemeo. Uwakomboe walio taabuni kati yetu, uwahurumie wanyonge, uwainue walioanguka, ujidhihirishe kwa wahitaji, uwaponye wagonjwa, uwarudishe waliojitenga na taifa lako, uwashibishe wenye njaa, uwafungue wafungwa wetu, uwaimarishe walio dhaifu, uwatulize walio duni.

Mataifa yote wapate kujua ya kuwa ndiwe Mungu, wewe peke yako, na ya kuwa Yesu Kristo ni Mwanao nasi tu wako na kondoo wa malisho yako.

                                     

2. Maandishi yake kwa Kiswahili

 • Didakè yaani Mafundisho ya Mitume Kumi na Wawili na Waraka wa Mt. Klementi kwa Wakorinto, tafsiri ya B. Santopadre n.k. – ed. E.M.I. – Bologna Italia 1990 – ISBN 88-307-0321-4
                                     

3. Marejeo

 • Meeks, Wayne A. 1993. The origins of Christian morality: the first two centuries. New Haven: Yale Univ. Press. ISBN 0-300-05640-0.
 • Richardson, Cyril Charles 1943. Early Christian Fathers, The Library of Christian Classics. Philadelphia: Westminster Press.
 • Loomis, Louise Ropes 1916. The Book of Popes Liber Pontificalis. Merchantville, NJ: Evolution Publishing. ISBN 1-889758-86-8.
 • 1937 The First Epistle of Clement to the Corinthians. London: Society for the Promotion of Christian Knowledge.
 • Lightfoot, J.B. 1890. The Apostolic Fathers. London: Macmillan.
 • 1964 The Apostolic Fathers. New York: Nelson.
 • Staniforth, Maxwell 1968. Early Christian writings. Baltimore: Penguin.
                                     

4. Viungo vya nje

 • Hieromartyr Clement the Pope of Rome Eastern Orthodox icon and synaxarion
 • "Saint Clement I." Encyclopædia Britannica Online.
 • Patron Saints Index: Pope Saint Clement I Archived Novemba 22, 2008 at the Wayback Machine.
 • St. Clement page Archived Oktoba 2, 2012 at the Wayback Machine. at Christian Iconography
 • "Here Followeth the Life of St. Clement" Archived Machi 13, 2013 at the Wayback Machine. in the Caxton translation of the Golden Legend
 • Two Epistles Concerning Virginity.
 • Kuhusu Papa Klementi I katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki
 • Opera Omnia
                                     
 • Papa Adrian I alikuwa Papa kuanzia tarehe 9 Februari 772 hadi kifo chake tarehe 25 Desemba 795. Jina la baba yake lilikuwa Theodorus. Alimfuata Papa Stefano
 • Papa Adeodato I pia aliitwa Deusdedit alikuwa Papa kuanzia tarehe 13 Novemba 615 hadi kifo chake tarehe 8 Novemba 618. Jina la baba yake lilikuwa Stephanus
 • Papa Anastasio I alikuwa Papa kuanzia tarehe 27 Novemba 399 hadi kifo chake mwezi wa Desemba 401. Alimfuata Papa Siricius akafuatwa na mwanae Papa Inosenti
 • Papa Innocent I alikuwa Papa kuanzia Desemba 401 hadi kifo chake tarehe 12 Machi 417. Alimfuata Papa Anastasio I baba yake, akafuatwa na Papa Zosimus
 • Papa Silvester I alikuwa Papa kuanzia tarehe 31 Januari 314 hadi kifo chake tarehe 31 Desemba 335. Alimfuata Papa Miltiades akafuatwa na Papa Marko. Mtoto
 • Papa Damaso I takriban 304 11 Desemba 384 alikuwa Papa kuanzia mwezi wa Oktoba 366 hadi kifo chake. Jina lake la kuzaliwa pia lilikuwa Damasus. Alimfuata
 • Papa Pelagio I alikuwa Papa kuanzia tarehe 16 Aprili, 556 hadi kifo chake tarehe 3 Machi, 561. Alimfuata Papa Vigilio akafuatwa na Papa Yohane III. Ekonomou
 • Papa Felix I alikuwa Papa kuanzia tarehe 5 Januari 269 hadi kifo chake tarehe 30 Desemba 274. Alimfuata Papa Dionysius akafuatwa na Papa Eutychian. Tangu

Users also searched:

...
...
...