Back

ⓘ Amandi wa Bordeaux
                                     

ⓘ Amandi wa Bordeaux

Amandi wa Bordeaux alikuwa askofu wa 13 wa mji huo kuanzia mwaka 403 hadi 410 hivi, tena kuanzia 420 hivi kifo chake.

Alijitahidi kuinjilisha jimbo lake akabatiza Paulino wa Nola ambaye aliandika mara nyingi juu yake kwa sifa.

Alipinga uzushi wa mmonaki Prisiliani na wa Gnosi.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Juni.