Back

ⓘ Atoni wa Pistoia
Atoni wa Pistoia
                                     

ⓘ Atoni wa Pistoia

Atoni wa Pistoia, O.S.B. alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 1135.

Kabla ya hapo alikuwa mmonaki wa urekebisho wa Vallombrosa na alifanywa abati mwaka 1105.

Aliandika maisha ya mtakatifu Yohane Gualberto na ya askofu Bernardo wa Uberti.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Mei.