Back

ⓘ Austregesili
Austregesili
                                     

ⓘ Austregesili

Austregesili anakumbukwa kama askofu wa Bourges kuanzia mwaka 612 hadi kifo chake.

Baada ya kufanya kazi katika ikulu, alikwenda kujiunga na monasteri akawa abati hadi alipoteuliwa kuwa askofu.

Hapo alionyesha upendo wa pekee kwa maskini, mayatima, wagonjwa na waliohukumiwa kufa.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Mei.