Back

ⓘ Barsimeo wa Edessa
                                     

ⓘ Barsimeo wa Edessa

Barsimeo wa Edessa alikuwa askofu wa Edessa, leo nchini Uturuki.

Aliwahi kupigwa fimbo kutokana na dhuluma ya kaisari Decius 249-251 lakini hakuuawa, bali alirudi jimboni mwake na kuliongoza kwa bidii hadi kifo chake. Kati ya watu aliowaongoa kuna Sharbel na Bebaya.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Januari.