Back

ⓘ Aldegunda
Aldegunda
                                     

ⓘ Aldegunda

Aldegunda, O.S.B., alikuwa mwanamke aliyeanzisha monasteri pacha na kuziongoza kama abesi.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu bikira.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Januari.

                                     

1. Maisha

Mtoto wa wazazi wa koo mashuhuri, aliongokea Ukristo akabatizwa alifuatwa na baba yake, ambaye akawa baadaye mtakatifu Walbert. Pia mama yake Bertila na dada yake waltrude ni watakatifu.

Baada ya kukataa kuolewa, alitawa.

Alivumilia kwa ushujaa maumivu ya saratani ya matiti ambayo ikaja kumuua.