Back

ⓘ Bonito wa Lyon
Bonito wa Lyon
                                     

ⓘ Bonito wa Lyon

Bonito wa Lyon au Bonitus wa Clermont aliwahi kuwa na vyeo mbalimbali muhimu, kama vile chansela wa mfalme, gavana wa Marseilles na hatimaye kwa miaka kumi askofu wa Auvergne baada ya kifo cha kaka yake Avitus.

Baada ya kungatuka, alikwenda kuishi miaka 4 monasterini na hatimaye akaenda kuhiji Roma. Wakati wa kurudi Ufaransa alifariki.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.