Back

ⓘ Albano Roe
Albano Roe
                                     

ⓘ Albano Roe

Albano Roe, O.S.B. alikuwa Mkristo wa Kanisa la Anglikana kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki pamoja na ndugu yake James.

Baada ya kuhamia Ufaransa, aliingia seminari 1607 kwa kengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali, lakini alifukuzwa kwa tabia yake 1610. Baadaye alijiunga na monasteri ya Wabenedikto 1613 na kupewa daraja ya upadri 1615.

Hapo alirudi London lakini alifukuzwa baada ya muda mfupi. Alirudi tena mwaka 1618 akafungwa hadi 1623. Miaka miwili baadaye akarudi tena akafungwa kwa miaka 17, lakini gereza halikuwa na nidhamu kali, hivyo akaweza kufanya utume wake mchana na kurudi kulala jela usiku.

Mwaka 1641 alihamishiwa gereza lingine alipokataa kuasi na kwa ajili hiyo mwaka uliofuata aliuawa kwa kunyongwa chini ya sheria.

Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39.

Sikukuu yake ni tarehe 21 Januari.

                                     

1. Marejeo

  • Bishop Challoner, Memoirs of Missionary Priests and other Catholics of both sexes that have suffered death in England on religious accounts from the year 1577 to 1684 Manchester 1803
                                     

2. Viungo vya nje

  • Story of Saint Alban Roe on Ampleforths website
  • "Bartholomew Roe". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
  • Patron Saints Index: Saint Alban Bartholomew Roe