Back

ⓘ Basiano wa Lodi
Basiano wa Lodi
                                     

ⓘ Basiano wa Lodi

Basiano wa Lodi alikuwa askofu wa mji huo wa Italia Kaskazini kuanzia mwaka 373 hadi kifo chake.

Kama kijana aliyekwenda Roma kwa masomo, na huko aliongokea dini ya Ukristo. Baba yake alitaka aasi na kurudi nyumbani, lakini yeye alikataa na kukimbilia Ravenna.

Baada ya kuchaguliwa askofu, alishiriki mtaguso wa Akwileia 381 na labda hata mtaguso wa Milano 390. Alisaini pamoja na rafiki yake askofu Ambrosi wa Milano barua kwa Papa Sirisi.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Januari.