Back

ⓘ Andrea Bessette
Andrea Bessette
                                     

ⓘ Andrea Bessette

Andrea Bessette, alikuwa bradha wa shirika la Msalaba Mtakatifu nchini Kanada.

Alizaliwa katika familia ya kawaida yenye watoto wengi, akawahi kubaki yatima na kukabidhiwa kwa utunzaji wa shangazi. Alifanya kazi katika kiwanda cha nguo huko Kanada na Marekani.

Mwaka 1870 aliingia utawani akapewa kazi ya bawabu wa ofisi ya chuo cha Notre-Dame huko Montreal.

Alikuwa na sifa kama mponyaji.

Alithibitishwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri mnamo 1982, Papa Benedikto XVI akamtangaza mtakatifu tarehe 17 Oktoba 2010.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.