Back

ⓘ Andrea Corsini
Andrea Corsini
                                     

ⓘ Andrea Corsini

Andrea Corsini, O.Carm. alikuwa Mkarmeli wa Italia aliyehudumia kama askofu wa Fiesole tangu mwaka 1349 hadi kifo chake.

Corsini aliishi vibaya hadi karipio la mama yake lilipomfanya aamue kuingia utawani awe padri Mkarmeli.

Baada ya kushika nafasi mbalimbali shirikani, alikubali kwa shida uaskofu akiongeza juhudi zake za kiroho na matendo ya huruma kwa maskini.

Tangu kale aliheshimiwa na waumini na hatimaye Papa Eugenio IV alimtangaza mwenye heri tarehe 21 Aprili 1440 na Papa Urban VIII alimtangaza mtakatifu tarehe 22 Aprili 1629.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.