Back

ⓘ Pages using ISBN magic links
                                               

2 Pallas

2 Pallas ni asteroidi ya pili iliyowahi kutambuliwa katika Mfumo wa Jua. Iligunduliwa na mtibabu na mwanaastronomia Mjerumani Heinrich Wilhelm Matthäus Olbers mnamo 28 Machi 1802. Jina la "2 Pallas" inaunganisha jina lililotolewa na Olbers, pamoja na namba ya asteroidi iliyojulikana. Jina lenyewe limanrejelea Pallas Athena aliyeabudiwa kama mungu katika dini ya Ugirki ya Kale. 2 Pallas ina masi inayokadiriwa kuwa asilimia 7% ya masi yaote ya ukanda wa asteroidi. Ni asteroidi kubwa ya tatu kulingana na masi yake, na ya pili kwa kuangalia kipenyo chake. Umbo lake linafanana na duaradufu yeny ...

                                               

2001 (albamu)

2001 ni jina la albamu ya pili ya msanii na mtayarishaji wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani - Dr. Dre. Albamu ilitolewa mnamo tar. 16 Novemba, 1999, kupitia studio za Interscope Records. Hili ni toleo la pili baada ya albamu ya kwanza ya Dr. Dre The Chronic. Kimsingi ilitayarishwa na Dr. Dre na Mel-Man, na Lord Finesse, na kushirikisha michango kadha wa kadha kutoka kwa marapa wengine kama vile Hittman, Snoop Dogg, Kurupt, Xzibit, Nate Dogg, na Eminem. 2001 inadhihirisha upanuzi katika kuandaa midundo ya G-funk ambayo ina maudhui ya gangsta rap au rap ya kihuni au kisela - kukiwa ...

                                               

A Man of the People

A Man of the People ni riwaya ya 1966 iliyoandikwa na Chinua Achebe. Ni riwaya ya nne ya Achebe. Kitabu hicho kinaelezea hadithi ya vijana aliyeelimika aitwaye Odili, na vita vyake na Chief Nanga, mwalimu wake wa zamani ambaye aliingia katika siasa katika nchi ya kisasa ya Afrika isiyotajwa. Odili anawakilisha kizazi kipya; Nanga anawakilisha desturi ya Nigeria. Mwisho wa kitabu unaisha kwa mapinduzi ya kijeshi, sawa na maisha halisi ya Johnson Aguiyi-Ironsi, Chukwuma Kaduna Nzeogwu na Yakubu Gowon. Sawa na maisha halisi ya Johnson Aguiyi-Ironsi, Chukwuma Kaduna Nzeogwu na Yakubu Gowon.

                                               

A New Day.

A New Day. ilikuwa aina ya sanaa za nyimbo zilizoimbwa na Céline Dion katika ukumbi wa viti 4000 iliyopo Caesars Palace mjini Las Vegas. Iliundwa na kuongozwa na Franco Dragone (anayojulikana kwa kazi yake kwa Cirque du Soleil na ikaanza tarehe 25 Machi 2003. A New Day. ilianzisha mfumo mpya wa maonyesho ya burudani, kwa kuchanganya nyimbo, utendaji sanaa, ubunifu, na teknolojia. Ilichukua muda wa dakika 90. Dion alipewa mkataba wa miaka mitatu hapo awali, lakini kwa ajili ya mafanikio yake, yeye aliendelea kuimba kwa miaka miwili zaidi. A New Day. ilimalizika 15 Desemba 2007, baada ya kui ...

                                               

Aaliyah

Aaliyah Dana Haughton alikuwa msanii wa rekodi, mwigizaji, na mwanamitindo kutoka nchini Marekani. Alijulikana sana kwa jina la kisanii kama Aaliyah. Aaliyah alizaliwa mjini Brooklyn, New York, na kukulia mjini Detroit, Michigan. Wakati wa umri wake wa awali, amepata kuonekana kwenye kipindi cha televisheni cha Star Search na kutumbuiza kwenye onyesho hilo na Gladys Knight. Akiwa na umri wa miaka 12, Aaliyah aliingia mkataba na Jive Records na Blackground Records na mjomba wake, Barry Hankerson. Akamtambulisha kwa R. Kelly, ambaye baadaye akaja kuwa mshauri wake, vilevile mtunzi na mtayari ...

                                               

Abd al Aziz al-Amawi

Abd al-Aziz al-Amawi alikuwa mtaalamu Mwislamu aliyefuata dhehebu la Washafii na mafundisho ya Ashari. Alikuwa shehe wa Wasufi wa jumuiya ya Qadiriya alikoanzisha tawi lake. Alikuwa mshauri wa masultani mbalimbali wa Zanzibar.

                                               

Abobaku

Abobaku ni filamu fupi ya mwaka 2010 iliyoandikwa na kutayarishwa na Femi Odugbemi na kuongozwa na Niji Akanni. Mwaka 2010 filamu hii ilishinda katika tamasha la Zuma Film Festival kama filamu bora fupi inayoeleweka zaidi na tarehe 10 April 2010 ilipata tuzo nyingine ya 6th Africa Movie Academy Awards Tuzo zilifanyika katika kituo cha Gloryland Culural Centre katika mji wa Yenagoa, Bayelsa State, Nigeria.

Ada (lugha ya programu)
                                               

Ada (lugha ya programu)

Ada ni lugha ya programu. Iliundwa na Jean Ichbiah na CII Honeywell Bull na ilianzishwa tarehe 1 Februari 1980. Iliundwa ili kuumba programu na kurahisisha kujifunza lugha za programu. Leo tunatumia Ada 2012: Tucker Taft. Ilivutwa na Pascal. Inaitwa Ada kwa heshima ya Ada Lovelace ambaye alikuwa mwanaprogramu wa kwanza.

                                               

Adalardo wa Corbie

Adalardo wa Corbie alikuwa mjukuu wa Karolo Nyundo kama Karolo Mkuu. Alijiunga na monasteri na kuwa abati, lakini kwa muda fulani alitakiwa pia kuwa waziri mkuu wa ufalme wa Italia. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Januari.

                                               

Adoni wa Vienne

Adoni wa Vienne, O.S.B. alikuwa mmonaki mwanahistoria na hatimaye askofu mkuu wa Vienne kuanzia mwaka 850 hadi kifo chake Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Desemba.

                                               

Afrodisi wa Misri

Afrodisi wa Misri alikuwa padri wa Misri aliyeuawa kwa ajili ya imani yake pamoja na waumini 30. Hayajulikani mengine kuhusu historia yake. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Aprili.

                                               

Agapio, Sekondino na wenzao

Agapio, Sekondino na wenzao walikuwa Wakristo waliouawa kwa ajili ya imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Valeriani. Agapio na Sekondino walikuwa maaskofu, Emiliani alikuwa askari, Tertula na Antonia walikuwa mabikira. Pia aliuawa mama mmoja pamoja na watoto wake pacha. Wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini. Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 4 Mei.

                                               

Agatoni mkaapweke

Agatoni mkaapweke alikuwa mfuasi wa Antoni Mkuu anayehesabiwa na Kanisa kuwa baba wa umonaki, ingawa kihistoria si wa kwanza kushika mtindo huo wa maisha katika Ukristo. Anaheshimiwa tangu zamani sana kama mtakatifu. Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 21 Oktoba kila mwaka.

                                               

Agoardi na wenzake

Agoardi na wenzake, akiwemo Ajibati walikuwa Wakristo wengi waliouawa kwa ajili ya imani yao. Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini. Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 24 Juni.

Aishwarya Rai
                                               

Aishwarya Rai

Mshindi 2017 – Vogue Beauty Awards – Most Beautiful Global Indian Icon of the decade 2011 – Vogue Beauty Awards – Global Beauty Icon award. 2017 – Vogue Women Of The Year Awards – Influencer of the Decade

Alfonso wa Orozco
                                               

Alfonso wa Orozco

Alfonso wa Orozco, O.S.A. alikuwa padri wa shirika la Waaugustino aliyepata umaarufu kwa mahubiri yake na kwa maisha ya kiroho. Papa Leo XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 15 Januari 1882, halafu Papa Yohane Paulo II akamtangaza mtakatifu tarehe 19 Mei 2002. Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe ya kifo chake.

Users also searched:

...
...
...