Back

ⓘ Tambarare kuu za Marekani
Tambarare kuu za Marekani
                                     

ⓘ Tambarare kuu za Marekani

Tambarare kuu za Marekani ni eneo kubwa la nchi hiyo lisilo na milima katika sehemu za kati na za magharibi za Marekani. Sehemu ya kaskazini inaingia ndani ya Kanada.

Upande wa magharibi zinaishia kwenye milima ya Rocky Mountains. Upande wa mashariki tambarare hizi zinapakana na maeneo ambako usimbishaji unaruhusu kustawi kwa misitu.

Majimbo yafuatayo ni sehemu za tambarare kuu:

  • Maeneo yote ya Kansas, Nebraska, Dakota Kaskazini na Dakota Kusini Marekani
  • Sehemu za kusini za Alberta, Saskatchewan na Manitoba Kanada
  • Sehemu za Colorado, Montana, New Mexico, Oklahoma, Texas na Wyoming Marekani

Tabianchi huwa na miezi ya joto kali pamoja na miezi ya baridi sana. Uoto asilia wa nchi ulikuwa manyasi tu, maana mvua haitoshi kwa miti mingi.

Kabla ya kuja kwa Wazungu huko Marekani, tambarare kuu zilikuwa na ngombe mwitu aina ya baisoni kwa mamilioni waliowindwa na Maindio wahamaji na kuwa chakula chao kikuu.

Baisoni waliuawa kwa makusudi na Wamarekani weupe waliotaka kuondoa msingi wa kiuchumi wa Maindio na kutumia maeneo yao kwa kilimo. Sasa ni kitovu cha mazao ya nafaka kama mahindi na ngano ambazo hulisha mifugo na watu.

                                     

1. Tovuti za Nje

  • Kansas Heritage Group: Nyumba za Wenyeji, Uhifadhi, Maua, na Utafiti
  • Chuo Kikuu cha Jimbo la Dakota Kaskazini: Hadithi ya Jiografia ya Tarafa Kubwa Archived Machi 5, 2009 at the Wayback Machine.
  • Chuo Kikuu cha Nebraska-Lincoln: Utafiti Mkuu wa Matawi
  • Maktaba ya Congress: Matawi mazuri

Users also searched:

...
...
...