Back

ⓘ Kordilera ya Amerika
Kordilera ya Amerika
                                     

ⓘ Kordilera ya Amerika

Kordilera ya Amerika ni mlolongo wa safu za milima kunjamano unaopita katika Amerika Kaskazini hadi Amerika Kusini upande wa magharibi kufuatana na pwani ya Bahari Pasifiki. Unaendelea hadi Antaktiki ya magharibi. Kordilera ni jina la Kihispania inayomaanisha safu ya milima.

Kaskazini mfumo huo wa milima unaanzia Alaska kaskazini hadi kusini, mlolongo huu wa mwingiliano unaoingiliana na safu sambamba huanza huko Alaska unapita Yukon na British Columbia na kuendelea katika safu za Rocky Mountains.

Huko Mexico milima ya kordilera inaendelea kupitia Sierra Madre ya Mashariki na Sierra Madre ya Mashariki, pamoja na milima ya rasi ya Baja California.

Kusini mwa Meksiko milima ya kordilera inaendelea katika Amerika ya Kati, yaani huko Guatemala, Honduras, Nicaragua, Costa Rica na Panama.

Kuanzia huko inaendelea upande wa kusini kama Milima ya Andes ya Amerika Kusini.

Katika nchi za Kolombia, Venezuela, Ekuador, Peru, Bolivia, Argentina, na Chile Andes inaendelea kama mfumo wa safu zinazoenea kandokando hadi ncha ya Amerika Kusini huko Tierra del Fuego.

Mfumo huo unaendelea chini ya bahari ya Kusini hadi kuonekana tena kwenye milima ya Grahamland kwenye Rasi ya Antaktiki.

Users also searched:

...