Back

ⓘ Augusto wa Caserta
                                     

ⓘ Augusto wa Caserta

Augusto wa Caserta alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo wa Italia Kusini lakini alikuwa mzaliwa wa Afrika Kaskazini.

Baada ya kuteswa na Wavandali Waario kwa sababu ya imani yake, alifukuzwa akiwa na wenzake 12, inasemekana kwa kuachwa baharini katika meli mbovu isiyoweza kuendeshwa.

Labda wakati huo alikuwa padri au askofu tayari. Baada ya kufika Italia, aliongoza jimbo la Caserta.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Septemba.