Back

ⓘ Bahari ya Weddell
Bahari ya Weddell
                                     

ⓘ Bahari ya Weddell

Bahari ya Weddell ni sehemu ya Bahari ya Kusini iliyopo katika hori kubwa baina ya Rasi Antaktiki na Nchi ya Coats. Sehemu kubwa ya eneo lake imefunikwa na barafu ya kudumu. Upana kwenye mdomo wa hori ni karibu km 2.000, eneo hilo ni karibu kilomita za mraba milioni 2.8. Kina chake ni baina ya mita 500 hadi 5.000.

Bahari hiyo ilipewa jina la nahodha Mwingereza na mwindaji wa sili James Weddell aliyeingia katika bahari hiyo mnamo 1823 akafika hadi latitudo ya kusini ya 74. Sili wa Weddell ni moja ya wanyama ambao wanaishi katika eneo hilo.

Argentina nchi iliyo karibu zaidi, Chile na Ufalme wa Muungano wanashindana kuhusu usimamizi wa sehemu hii.

Users also searched:

...