Back

ⓘ Arkinimo
                                     

ⓘ Arkinimo

Arkimino alikuwa Mkristo Mkatoliki wa ukoo bora ambaye alikatwa kichwa na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Genseriki aliyekuwa Mwario.

Habari zake zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Machi pamoja na wenzake Armogaste na Saturus.