Back

ⓘ Androniko na Athanasia
                                     

ⓘ Androniko na Athanasia

Androniko na Athanasia walikuwa Wakristo wa Antiokia ya Syria kati ya karne ya 4 na ya 5.

Mume na mke, walipofiwa watoto wao wawili, walikubaliana kutengana wakaenda kuishi kwa sala na toba katika Misri Kusini.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Oktoba.