Back

ⓘ Mlangobahari wa Magellan
Mlangobahari wa Magellan
                                     

ⓘ Mlangobahari wa Magellan

Mlangobahari wa Magellan ni nafasi ya kupita kwa chombo cha bahari kutoka Atlantiki hadi Bahari Pasifiki bila kuvuka Rasi ya Hoorn.

Ni njia nyembamba ya maji inayopita kati ya Amerika Kusini bara na Tierra del Fuego Nchi ya moto. Pwani zake ni za Argentina upande wa kaskazini na Chile upande wa kusini. Nchi hizo mbili zilivutana kwa muda mrefu ni nani anayestahili kusimamia mlangobahari huu, sasa iko chini ya Chile.

Jina lilitolewa kwa heshima ya nahodha na mpelelezi Mreno Ferdinand Magellan aliyepita hapa mara ya kwanza.

Si njia nyepesi kwa meli na jahazi maana kuna dhoruba za mara kwa mara na ukungu mwingi.

Users also searched:

...
...
...