Back

ⓘ Makari wa Aleksandria
Makari wa Aleksandria
                                     

ⓘ Makari wa Aleksandria

Makari wa Aleksandria alikuwa mmonaki maarufu katika jangwa la Nitria.

Alikuwa kijana zaidi kidogo kuliko Makari Mkuu, ndiyo sababu anaitwa pengine Makari Kijana.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Januari au 1 Mei.

                                     

1. Maisha

Mzaliwa wa Aleksandria, alikuwa mfanyabiashara hadi umri wa miaka 40, alipobatizwa na kwenda kuishi jangwani.

Baada ya miaka kadhaa, alipewa upadrisho na kufanywa priori wa monasteri fulani, katika mlima Nitria.

Mwaka 335, Makari alikwenda kuishi peke yake katika jangwa la el-Natroun akiwa mkuu wa wakaapweke zaidi ya elfu tano.

Miujiza mingi inasimuliwa kuwa ilifanywa kwa maombezi yake.

Alipofikia umri wa miaka 73 Makari alipelekwa uhamishoni na Kaisari Valens, pamoja na Makari Mkuu wakaishi katika kisiwa fulani ambacho walifaulu kukiinjilisha.

                                     

2. Viungo vya nje

  • Butler, Alban. The Lives of the Saints, Volume I, 1866
  • Healy, Patrick. "Macarius." The Catholic Encyclopedia. Vol. 16 Index. New York: The Encyclopedia Press, 1914
                                     
  • Makari I wa Aleksandria alifariki 953 kuanzia mwaka 933 hadi kifo chake alikuwa Patriarki wa Aleksandria Misri na Papa wa 59 wa Kanisa la Kikopti
  • Makari wa Aleksandria alifia dini 250 hivi alikuwa Mkristo wa mji huo nchini Misri ambaye aliuawa kikatili wakati wa dhuluma ya kaisari Decius. Inasemekana
  • Makari II wa Aleksandria alifariki 14 Septemba 1128 kuanzia mwaka 1102 hadi kifo chake alikuwa Patriarki wa Aleksandria Misri na Papa wa 69 wa Kanisa
  • watakatifu Jermaniko wa Filadelfia, Ponsyano wa Spoleto, Mario, Martha, Audifas na Abako, Makari mkuu, Makari wa Aleksandria Basiano wa Lodi, Liberata na
  • Makari Mkuu 300 hivi - 391 alikuwa mkaapweke na padri wa Misri. Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama
  • Misri Makari wa Aleksandria Makari Kijana Misri Makari wa Aleksandria mfiadini Misri Makari wa Fayum, Misri Makari wa Libya, Misri Makroni wa Thoni
  • Makari wa Libya alifia dini 250 hivi alikuwa Mkristo mwenye asili ya Libya ambaye alichomwa moto huko Aleksandria Misri kwa ajili ya imani yake wakati

Users also searched:

...
...
...