Back

ⓘ Mdudu Mabawa-vigamba
Mdudu Mabawa-vigamba
                                     

ⓘ Mdudu Mabawa-vigamba

Wadudu mabawa-vigamba ni wadudu wadogo hadi wakubwa wa oda Lepidoptera katika nusungeli Pterygota. Jina ni tafsiri ya jina la kisayansi. Wadudu hawa wanajulikana kama vipepeo na nondo.

Wadudu hawa wana mabawa kama viwambo, isipokuwa spishi kadhaa ambazo zina mabawa yaliyopunguka au hazina mabawa kabisa. Kinyume na wadudu mabawa-viwambo kwa kawaida mabawa yao yamefunikwa kwa vigamba ambavyo kweli ni manyoya yaliyofanyika kuwa bapa. Lakini mabawa ya spishi kadhaa yana sehemu bila vigamba zilizo nyangavu kwa hivyo k.m. Nondo mkia-mshale mwangavu.

Sehemu za kinywa za spishi nyingi zimetoholewa kuwa mrija mrefu sana unaoitwa ulimi au proboski. Mrija huo hutumiwa kufyonza mbochi au viowevu vingine. Lakini spishi za Zeugloptera bado zina sehemu za kutafuna kama ndugu wao wa oda Trichoptera Wadudu mabawa-manyoya.

Wachanga wa vipepeo na nondo huitwa viwavi. Hawafanani na wapevu kwa sababu hawana mabawa, wana sehemu za kinywa za kutafuna na wana miguu bandia kwenye fumbatio licha ya miguu sita ya kweli kwenye toraksi. Kwa kawaida viwavi hula majani ya mimea na mara nyingi shina pia na pengine hata matunda. Spishi fulani za viwavi hula wadudu wengine na nyingine ni vidusia.

                                     

1. Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki

 • Colotis euippe Round-winged orangetip
 • Euphaedra rattrayi Orange forester
 • Precis octavia Gaudy commodore
 • Sarangesa motozi Elfin skipper
 • Coeliades forestan Striped policeman
 • Spodoptera exempta, Kiwavi-jeshi wa Afrika African armyworm
 • Cephonodes hylas, Nondo Mkia-mshale Mwangavu Pellucid hawk moth
 • Colias electo African clouded yellow
 • Plutella xylostella, Nondo Mdogo wa Kabichi Diamondback moth
 • Helicoverpa armigera, Nondo wa Nyanya Cotton bollworm
 • Actizera stellata Clover blue
                                     

2. Mwainisho

 • Familia ya juu Agathiphagoidea
 • Nusuoda Aglossata
 • Oda za chini
 • Acanthoctesia
 • Neopseustina
 • Dacnonypha
 • Lophocoronina
 • Exoporia
 • Nusuoda Glossata
 • Heteroneura
 • Nusuoda Heterobathmiina
 • Familia ya juu Heterobathmioidea
 • Nusuoda Zeugloptera
 • Familia ya juu Micropterigoidea

Users also searched:

...
...
...