Back

ⓘ Mdudu Mabawa-viwambo
Mdudu Mabawa-viwambo
                                     

ⓘ Mdudu Mabawa-viwambo

Wadudu mabawa-viwambo ni wadudu wadogo sana hadi wakubwa kiasi wa oda Hymenoptera katika nusungeli Pterygota. Jina ni tafsiri ya jina la kisayansi. Wadudu hawa wanajulikana sana kama nyuki, nyigu, dondora na sisimizi k.m.

Takriban spishi zote zina mabawa kama viwambo, lakini spishi nyingine au wana wa spishi nyingine kama sisimizi hawana mabawa. Kwa kawaida majike wana mrija wa kutaga mayai unaoweza kuingiza mayai ndani ya kidusiwa au katika mahali palipo ngumu kufikia. Katika spishi nyingi mrija huo umetoholewa kuwa mwiba.

Spishi za nusuoda Apocrita zina kiuno chembamba sana lakini zile za Symphyta zina kiuno kipana.

                                     

1. Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki

 • Polistes fastidiosus, Mavu
 • Arge taitaensis, Mdudu-msumeno
 • Megaponera analis, Sungusungu
 • Xylocopa caffra, Nyuki-bungu njano
 • Vespa orientalis, Dondora
 • Sceliphron spirifex, Bunzi mweusi-na-njano
                                     

2. Mwainisho

 • Anaxyeloidae
 • Nusuoda Symphyta
 • Xyeloidea
 • Pamphilioidea
 • Cephoidea
 • Tenthredinoidea
 • Siricoidea
 • Orussoidea
 • Familia za juu
 • Xiphydrioidea
 • Chrysidoidea Nyigu-kekeo n.k.
 • Familia za juu
 • Apoidea
 • Oda ya chini Aculeata
 • Vespoidea Dondora, mavu n.k.
 • Nusuoda Apocrita
 • Formicoidea Sisimizi
 • Evanioidea
 • Familia za juu
 • Stephanoidea
 • Megalyroidea
 • Trigonaloidea
 • Proctotrupoidea
 • Platygastroidea
 • Ceraphronoidea
 • Ichneumonoidea
 • Chalcidoidea
 • Cynipoidea
 • Oda ya chini Parasitica
 • Mymarommatoidea
 • Diaprioidea

Users also searched:

...
...
...