Back

ⓘ Alipius wa Thagaste
Alipius wa Thagaste
                                     

ⓘ Alipius wa Thagaste

Alipius wa Thagaste alikuwa askofu wa Tagaste mwaka 394. Inasemekana ndiye wa kwanza kujenga monasteri sehemu hiyo ya Afrika.

Kwa muda mrefu sana alikuwa rafiki wa Augustino wa Hippo akaungana naye katika kuongokea Kanisa Katoliki 386; Confessions 8.12.28 na katika maisha ya kiroho.

Karibu yote tunayoyajua juu yake yanatokana na kitabu cha Augustino juu ya maisha yake mwenyewe Maungamo Confessiones.

Papa Gregori XIII alimtangaza mtakatifu mwaka 1584.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Agosti.