Back

ⓘ Achilas wa Aleksandria
                                     

ⓘ Achilas wa Aleksandria

Achilas wa Aleksandria au Achilas Mkuu alikuwa Patriarki wa 18 wa Aleksandria alipokuwa amezaliwa katika karne ya 3.

Alipata umaarufu kwa ujuzi na maadili yake. Ndiyo sababu Theonas wa Aleksandria alimpa upadirisho na kumfanya mkuu wa Chuo cha Aleksandria baada ya Pierio kuhama.

Kwa pendekezo la mfiadini Petro I wa Aleksandria, alitawazwa kuwa mwandamizi wake kama Patriarki tarehe 24 Desemba 312 Baada ya kumrudisha Ario katika nafasi ya padri na mhubiri kwa kudhani ametubu, alifariki tarehe 26 Juni 313.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Wakopti kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Juni.