Back

ⓘ Krisogoni
Krisogoni
                                     

ⓘ Krisogoni

Krisogoni alikuwa mwanamume Mkristo wa Roma ya Kale ambaye aliuawa kwa sababu ya imani yake, inawezekana sana wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Wa kwanza wanaadhimisha sikukuu yake tarehe 24 Novemba, wa pili tarehe 22 Desemba pamoja na anayesemekana alikuwa mwanafunzi wake Anastasia wa Sirmio.

Katika Martyrologium Hieronymianum aliorodheshwa katika tarehe mbili tofauti: 31 Mei na 24 Novemba

Krisogoni ni kati ya watakatifu wanaotajwa katika Kanuni ya Kirumi.

                                     

1. Viungo vya nje

  • Saint of the Day, November 24: Saint Chrysogonus Archived Agosti 7, 2014 at the Wayback Machine. at SaintPatrickDC.org
  • Saint Chrysogonus at the Christian Iconography web site
  • Martyr Chrysogonus the Teacher of the Greatmartyr Anastasia Orthodox Synaxarion life of the saint
  • "Here Followeth the Life of S. Grysogone" from the Caxton translation of the Golden Legend
  • Kiitalia San Crisogono di Aquileia
                                     
  • Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Andrea Dung - Lac na wenzake, Krisogoni Firmina wa Amelia, Protasi wa Milano, Romano wa Blaye, Porsiani abati

Users also searched:

...
...
...