Back

ⓘ Thule
Thule
                                     

ⓘ Thule

Thule ilikuwa jina la kisiwa kwenye Atlantiki upande wa kaskazini wa Ulaya kilichotajwa na Pytheas wa Massilia, mpelelezi wa Ugiriki ya Kale katika karne ya 4 KK.

Haijulikani ni kisiwa gani alichotaja kama kilikuwa Iceland, Greenland au labda visiwa vya Faroe. Kuna hakika ya kwamba Pytheas alitaja mahali pa kaskazini kwa sababu aliandika ya kwamba "bahari inayoganda", yaani bahari inayofunikwa na barafu, ilianza safari ya siku 1 kutoka kule. Lakini haijulikani aliandika katika mwezi gani na uenezaji wa barafu baharini unabadilika pamoja na majira.

Kwa hiyo jina la Thule lilitumiwa katika Ulaya kwa kutaja mwisho wa Dunia iliyoweza kufikiwa na watu kabla ya kuingia katika maeneo ya barafu tupu.

Kutokana na imani hii jina la "Ultima Thule", ambalo ni Kilatini kwa "Thule ya mwisho" limekuwa namna ya kutaja "mwisho wa Dunia".

Katika mwezi wa Machi 2018 NASA iliamua kuita kiolwa cha angani katika Ukanda wa Kuiper "Ultima Thule" kwa sababu ni kiolwa cha mbali kabisa kitakachotembelewa na kipimaanga New Horizon mnamo tarehe 1 Januari 2019.

                                     

1. Kujisomea

  • Fotheringham, W.H. 1862. "On the Thule of the Ancients" pdf. Proceedings of the Society of Antiquaries of Scotland III: 491–503.
  • Burton, Richard F. 1875. Ultima Thule: Or, A Summer in Iceland. London, Edinburgh: W.P. Nimmo. Downloadable Google Books.
  • Gilberg, Rolf June 1976. "Thule" pfd. Arctic 29 2: 83–86.
. Retrieved 2008-10-30.
  • Joanna Kavenna, The Ice Museum: In Search of the Lost Land of Thule, London, Penguin, 2006. ISBN 978-0-14-101198-1
  • Thule, makala ktk Encyclopedia Britannica 1911
  • Pliny 1893. The Natural History of Pliny: Volume I. London, New York: George Bell & Sons, 352, notes on Book IV.
  • Pliny 1829. Histoire naturelle de Pline: Traduction Nouvelle: Vol III, Ajasson de Grandsagne trans. in French, Paris: C.L.F. Panckoucke, 337–338, notes on Book IV.

Users also searched:

thule bike rack 3, thule boot bike rack, thule pretoria,

...
...
...