ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 261
                                               

Ukanda wa asteroidi

Ukanda wa asteroidi ni mviringo wa asteroidi au miamba mikubwa na midogo na vumbi unaozunguka jua kati ya njia za Mirihi na Mshtarii katika mfumo wa jua letu. Umbali wake na jua ni eneo kati ya 2 hadi 3.4 vizio astronomia. Gimba kubwa katika ukan ...

                                               

Watroia

Watroia ni jina la makundi ya asteroidi zinazozunguka Jua zikitumia obiti ya Mshtarii. Huko hukaa kwa umbali wa pembe 60° na Mshtarii kwenye nukta msawazo ya obiti yake. Kwenye sehemu zao kani za uvutano wa Mshtarii na Jua zimefikia uwiano na kwa ...

                                               

Anufu ya Farasi

Anufu ya Farasi inayomaanisha" Pua la Farasi” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema kwa kawaida الأنف al-anfu inayom ...

                                               

Ayuki

Ayuki ni nyota angavu zadi katika kundinyota la Hudhi. Ni pia nyota angavu ya sita kabisa kwenye anga. Mwangaza unaoonekana ni 0.08 mag. Iko karibu na Dunia ikiwa umbali wa miaka nuru 43.

                                               

Hanaa ya Jauza

Hanaa ya Jauza ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Mapacha na nyota angavu ya 43 kwenye anga ya usiku.

                                               

Ibuti la Jauza

Jina la Ibuti la Jauza lilijulikana tangu karne nyingi kati ya mabaharia Waswahili waliotumia nyota hii kama msaada wa kukuta njia yao baharini wakati wa usiku. Asili ya jina ni Kiarabu إبط الجوزاء ibt al jauza na jina hili lilipokewa pia na wana ...

                                               

Jabuha Asadi

Gamma Leonis, also named Algieba Jabuha Asadi Jabuha Asadi ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Simba zamani Asadi, lat. Leo. Jabuha Asadi ni nyota maradufu iliyotambuliwa kuwa na angalau sayari moja.

                                               

Jina la Bayer

Jina la Bayer ni utaratibu wa kutaja nyota ulioanzishwa na mwanaastronomia Mjerumani Johann Bayer katika karne ya 17 na kutumiwa hadi leo kwa kutaja nyota angavu.

                                               

Jinaha la Ghurabu

Jinaha la Ghurabu ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Ghurabu Corvus. Iko karibu kiasi na nyota angavu ya Sumbula Spica katika Mashuke pia Nadhifa, lat. Virgo.

                                               

Jitu jekundu

Jitu jekundu ni jina la nyota kubwa zinazoonekana kungaa kwa rangi nyekundu. Mifano ni Dabarani katika kundinyota ya Tauri na Ibuti la Jauza kwenye Jabari. Wanaastronomia hufikiri ya kuwa karibu nyota zote zinapita kwenye ngazi ya jitu jekundu ka ...

                                               

Pembetatu ya Kiangazi

Pembetatu ya Kianganzi ni umbo la pembetatu kwenye anga la nusutufe ya kaskazini ya Dunia inayofanywa na nyota angavu tatu ambazo ni Vega katika Kinubi, Dhanabu ya Ukabu katika Dajaja na Tairi katika Ukabu. Pembetatu ya Kiangazi si kundinyota hal ...

                                               

Haumea

Haumea ni sayari kibete inayozunguka jua letu katika umbali mkubwa kwenye ukanda wa Kuiper. Ilitambuliwa mwaka 2004. Ina umbo la duaradufu; kipenyo chake baina ya ncha zake ni kilomita 1.138 lakini kipenyo kwenye ikweta ni kati ya km 2322 na km 1 ...

                                               

Darubini ya anga-nje

Darubini ya angani ni kifaa hasa darubini kilichorushwa katika anga la nje kwa kusudi la kuangalia na kupima violwa vya mbali kama vile nyota, sayari, galaksi na magimba mengine. Faida yake ni ya kwamba inaweza kuchungulia violwa hivi nje ya anga ...

                                               

Hubble (darubini)

Darubini ya Hubble ni darubini ya anga-nje iliyotengenezwa kwa ushirikianao baina ya taasisi za NASA na ESA kwa utafiti wa nyota. Ilipokea jina lake kwa heshima ya mwanaastronomia Edwin Hubble.

                                               

Paoneaanga pa Mount Palomar

Paoneaanga pa Mount Palomar ni kituo cha kuangalilia nyota kinachopatikana kwenye kimo cha mita 1706 juu ya milima ya Palomar takriban kilomita 80 upande wa kaskazini wa San Diego kwenye jimbo la Kalifornia, Marekani. Paoneaanga hapo palikuwa maa ...

                                               

Kituo cha umeme

Kituo cha umeme ni kiwanda ambako umeme unatengenezwa. Kwa kawaida kina idadi ya majenereta yanayotumia teknolojia ya sumakuumeme. Mara nyingi nguvu ya kuzungusha jenereta inapatikana kwa kutumia mvuke wa maji yaani mwendo wa mvuka huzungusha raf ...

                                               

Kuni

Kuni ni sehemu za mti uliokatwa zinazotumiwa kama fueli zikichomwa motoni kwa kupikia au pia kwa kupashia nyumba moto. Kwa kawaida kuni zinakusanywa penye miti kwa kutafuta sehemu ziliokauka au kwa kukata miti inayopasuliwa kuwa vipande vya ukubw ...

                                               

Mlipuko

Mlipuko ni tukio la kuachishwa kwa ghafla kwa kiwango kikubwa cha nishati ya joto, shinikizo au mwendo na kuongezeka kwa mjao. Tukio hili linaweza kusababishwa na mchakato wa kikemia, wa kifizikia. Matukio mengi ya asili yanaweza kufanya milipuko ...

                                               

RETScreen

Programu ya Usimamizi wa Nishati Safi ya RETScreen ni kifurushi cha programu kilichotengenezwa na Serikali ya Kanada. RETScreen Expert iliangaziwa mwaka 2016 katika Clean Energy Ministerial iliyofanyika San Francisco. Programu inapatikana katika ...

                                               

Tanuri la nyuklia

Tanuri la nyuklia ni mtambo ambamo mchakato mfululizo wa nyuklia unatokea. Mwatuko wa nyuklia huzalisha joto ambalo latumiwa kutengeneza umeme. Kuna aina mbalimbali za matanuri lakini kwa kawaida fueli ni ama urani-235 au plutoni-239.

                                               

Umememaji

Umememaji ni umeme unaozalishwa kwa kutumia mwendo wa maji. Kwa kawaida mwendo asilia wa maji huzuiliwa kwa kujenga lambo. Maji hufuata mvutano wa graviti yanataka kuteremka chini zaidi kila mahali yalipo kama kuna njia. Ukuta wa lambo huzuia mwe ...

                                               

Kivuli

Kivuli ni eneo lenye nuru kidogo katika mazingira yenye nuru zaidi. Kinapatikana nyuma ya gimba kinachoangazwa upande moja lakini kinazuia nuru kuendelea na hivyo kuunda eneo lenye giza au nuru kidogo nyuma yake. Kila kitu kisichopitisha nuru nda ...

                                               

Kijivu

Kijivu ni jina la aina za rangi zinazocheza kati ya nyeusi na nyeupe kwa kuzichanganya kwa kadiri tofautitofauti. Jina la rangi hiyo linatokana na majivu. Simiti ina rangi ya kijivu, pia tembo inaweza kuonyesha rangi hiyo.

                                               

Melanini

Melanini ni jina la pigmenti katika ngozi ya juu zinazofanya ngozi kuwa na rangi asilia fulani. Inapatikana pia katika nywele na sehemu za jicho. Kazi ya melanini inaaminiwa kupunguza athira ya mnururisho wa urujuanimno ing. ultraviolet katika nu ...

                                               

Nyekundu

Nyekundu ni moja ya rangi za pinde ya mvua. Inahesabiwa kati ya rangi kuu zinazoonekana kwa macho ya binadamu pamoja na buluu na manjano. Nyekundu ni rangi ya jua wakati wa kuzama. Ni pia rangi ya matunda mbalimbali na rangi ya damu. Inatazamiwa ...

                                               

Nyeusi

Nyeusi ni rangi tunayoona wakati jicho letu halipokei nuru, au miale ya nuru hafifu sana. Hapa ni sababu wengine husema nyeusi si rangi bali uhaba wa rangi zote. Kifizikia gimba lolote huonekana jeusi, kama haliakisii nuru hata kidogo. Nyeusi ni ...

                                               

Mtagusano sumakuumeme

Mtagusano sumakuumeme ni moja kati ya kani msingi wa ulimwengu. Mtagusano huu unasababisha mambo mengi tunayoyaona kila siku kama vile nuru, umeme na usumaku. Ni kani ya kimsingi pia kwa kuamulia tabia za molekuli na atomi.

                                               

Infraredi

Infraredi ni aina ya nuru isiyoonekana kwa macho ya kibinadamu lakini kuna wanyama wanaoweza kuiona. Inasikika kama joto. Kifizikia ni aina ya mnururisho wa sumakuumeme mwenye mawimbi marefu kuliko nuru ambayo inaonekana kwa binadamu na mawimbi a ...

                                               

Mnururisho sumakuumeme

Mnururisho sumakuumeme ni mnururisho wa mawimbi zinazounganisha uga sumaku na uga wa umeme na kubeba nishati. Mifano ya mawimbi sumakuumeme ni wimbiredio, mikrowevu, mawimbi ya joto, mawimbi ya urujuanimno, eksirei, na nuru inayoonekana kwetu. To ...

                                               

Spektra

Mfano wa spektra katika maisha ya kila siku ni rangi za upinde wa mvua. Hapo miale ya nuru inapinda wakati wa kupita kwenye matone madogo ya maji hewani. Sehemu za nuru zenye marudio zinapindishwa kwa namna tofauti wakati wa kubadilika kwa mazing ...

                                               

Frederick Duncan Michael Haldane

Frederick Duncan Michael Haldane ni mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Mwaka wa 2016, pamoja na David James Thouless na John Michael Kosterlitz, alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Alipewa tuzo kwa utafiti wa kinadharia katika maelez ...

                                               

John Michael Kosterlitz

John Michael Kosterlitz ni mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Mwaka wa 2016, pamoja na David James Thouless na Frederick Duncan Michael Haldane, alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Alipewa tuzo kwa utafiti wa kinadharia katika maelezo ...

                                               

David James Thouless

David James Thouless ni mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa aligundua m. Mwaka wa 2016, pamoja na Frederick Duncan Michael Haldane na John Michael Kosterlitz, alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Alipewa tuzo kwa utafiti wake wa k ...

                                               

Chaji ya umeme

Chaji ya umeme ni tabia ya mata na kila kitu huwa na chaji aina mbili ndani yake. Chaji hizi mbili ni kinyume zinaitwa chaji hasi na chaji chanya. Mara nyingi chaji haionekani kwa sababu hizi aina mbili za chaji zinajibatilishana. Lakini kama ida ...

                                               

Kikingaradi

Kikingaradi ni kifaa kinachofungiwa juu ya nyumba, minara au majengo marefu mengine. Kwa kawaida ni nondo nene ya metali ambayo inaunganishwa na waya inayoishia kwenye pao la metali lililochimbwa ardhini. Kazi ya kikingaradi ni kuvuta radi kwake ...

                                               

Maginetiti

Maginetiti ni madini yenye rangi nyeusi-kijivu yenye tabia ya sumaku. Kikemia ni oksidi ya feri yenye valensi za 2+ na 3+. Fomula yake ni Fe 3+ 2 Fe 2+ O 4. Inatokea mara nyingi kwa umbo la fuwele zenye urefu wa karibu sentimita 1 na kona 8. Kiwa ...

                                               

Uga sumaku

Uga sumaku ni nafasi karibu na sumaku au mkondo wa umeme ambamo kani inaathiri magimba ndani yake. Uga sumaku hauonekani kwa macho lakini unapimika. Kipimo cha SI kwa kutaja nguvu ya uga sumaku ni Tesla lakini mara nyingi kipimo cha kale cha Gaus ...

                                               

Duara

Duara ni umbo la mviringo bapa yaani katika tambarare linalofanana na herufi "o". Katika jiometria duara huelezwa kuwa mchirizo uliofungwa na umbali wa kila nukta ya mchirizo ni sawa kutoka kitovu cha duara. Mstari wa nje wa duara huitwa mzingo. ...

                                               

Duaradufu

Duaradufu ni neno la kutaja maumbo ya jiometria yanayofanana na duara. Kwa lugha ya kawaida ni umbo linalofanana na yai la ndege. Katika mazingira yetu obiti za sayari yaani njia ambako sayari zinazunguka jua huwa na umbo la duaradufu. Kwa maana ...

                                               

Eneo

Eneo katika elimu ya jiometria ni idadi inayoeleza ukubwa wa umbo bapa lenye upana na urefu. Kwa hiyo "eneo" linataja ukubwa wa gimba lenye wanda mbili. Hii inamaanisha maumbo ya jiografia bapa kama vile mraba, mstatili na duara lakini pia uso wa ...

                                               

Pembenne

Pembenne ni umbo bapa lenye pande nne. Kwa lugha nyingine ni pembenyingi yenye pembe nne. Pembenne hutokea kama nukta nne kwenye tambarare zaunganishwa kwa mistari inayofunga eneo ndani yao. Maumbo ya pekee ya pembenne ni mstatili, mraba, trapeza ...

                                               

Tufe

Tufe ni umbo la gimba linalofanana na mpira au chungwa. Lakini wala mpira wala chungwa ni tufe kamili. Katika elimu ya hisabati, hasa jiometri tufe ni jumla la nukta zote zilizopo na umbali uleule =rediasi, nusukipenyo kutoka nukta moja kitovu ch ...

                                               

Namba

Namba ni dhana na lugha inayotumiwa kutofautisha idadi au kupima kiwango. Namba zinazojulikana zaidi ni zile namba asilia kama vile 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10 na kadhalika. Utaalamu unaoshughulika habari za namba ni hasa hisabati pamoja na mat ...

                                               

Namba za Kiroma

Namba za Kiroma ni mfumo wa tarakimu kwa kuandika namba jinsi ulivyokuwa kawaida wakati wa Roma ya Kale na katika mwandiko wa Kilatini. Mfumo huu unaendelea kutumika hadi leo kwa namba za pekee, hasa katika muundo wa orodha ambako mgawanyo ni wa ...

                                               

Trilioni

Trilioni ni namba ambayo inamaanisha milioni mara elfu mara elfu moja, au milioni mara milioni na kuandikwa 1.000.000.000.000. Inafuata 999.999.999.999 na kufuatwa na 1.000.000.000.001. Inaweza kuandikwa pia kifupi 1 × 10 12.

                                               

Afrika ya Kati

Afrika ya Kati ni kanda la bara la Afrika iliyoko katikati ya bara. Katika hesabu ya Umoja wa Mataifa nchi 9 zifuatazo huhesabiwa kuwa sehemu zake: Afrika ya Kati kwa maana ya mpangilio ya UM ni nchi kusini ya jangwa Sahara, mashariki ya Afrika y ...

                                               

Afrika ya Kusini

Afrika ya Kusini ni ukanda ulioko kusini mwa bara la Afrika. Katika hesabu ya UM nchi 5 zifuatazo huhesabiwa kuwa sehemu za ukanda huo: Mara nyingi nchi zifuatazo zinatajwa pia kuwa nchi za Afrika ya Kusini: Komori, Morisi, Shelisheli, Mayotte na ...

                                               

Afrika ya Magharibi

Afrika ya Magharibi ni ukanda wa magharibi kwenye bara la Afrika. Kwa kawaida huhesabiwa humo nchi zilizo kati ya jangwa la Sahara na Bahari ya Atlantiki. Upande wa mashariki ukanda huu unaishia kwenye mstari kati ya mlima Kamerun na ziwa Chad. K ...

                                               

Bahari ya Mediteranea

Bahari ya Mediteranea ni bahari ya pembeni ya Atlantiki kati ya mabara ya Afrika, Ulaya na Asia ya Magharibi. Eneo lake ni takriban milioni 2.5 km². Kina chake kirefu ni 5.267 m. Ina kanda ya hali ya hewa ya pekee pamoja na mimea na wanyama. Neno ...

                                               

Demografia ya Afrika

Idadi ya wakazi wa Afrika imeongezeka sana katika karne ya mwisho, na kwa sababu hiyo wengi wao ni watoto na vijana, pia kwa sababu matarajio ya kuishi si ya miaka mingi. Katika miaka 1982–2009 idadi ya watu imekuwa maradufu tena ukihesabu miaka ...