ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 253
                                               

Ernst Ruska

Ernst August Friedrich Ruska alikuwa fundisanifu wa umeme kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa anajulikana kwa kubuni hadubini ya elektroni. Mwaka wa 1986, pamoja na Gerd Binnig na Heinrich Rohrer alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

Ernest Rutherford

Ernest Rutherford alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Utafiti wake hasa uliweka msingi kwa fizikia ya kiini. Mwaka wa 1908 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Leopold Ruzicka

Leopold Stefan Ruzicka alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uswisi. Baadhi ya utafiti mwingine alichunguza mfumo wa dawa za kuwaua wadudu. Mwaka wa 1939, pamoja na Adolf Butenandt alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Martin Ryle

Martin Ryle alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alichunguza mionzi ya nyota na kuvumbua darubini inayotumia mawimbi na mwangi wa redio. Mwaka wa 1966 alipewa cheo cha Sir cha Uingereza. Mwaka wa 1974, pamoja na Antony Hewish aliku ...

                                               

Paul Sabatier

Paul Sabatier alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ufaransa. Alichunguza sifa za elementi mbalimbali. Mwaka wa 1912 pamoja na Victor Grignard alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Abdus Salam

Abdus Salam alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Pakistan. Hasa alichunguza usumaku. Mwaka wa 1979, pamoja na Sheldon Glashow na Steven Weinberg alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia, Mwislamu wa kwanza kupata tuzo hiyo.

                                               

Frederick Sanger

Frederick Sanger alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alichunguza mfumo wa molekuli mbalimbali. Alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mara mbili, mwaka wa 1958 peke yake, na mwaka wa 1980 pamoja na Paul Berg na Walter Gilbert.

                                               

Arthur Schawlow

Arthur Leonard Schawlow alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Kama mtoto na kijana aliishi na kusoma nchini Kanada kabla hajarudi Marekani. Hasa alichunguza mnururisho na kubuni leza alipofanya kazi pamoja na Charles Townes. Mwaka wa 1981 ...

                                               

Robert Schrieffer

John Robert Schrieffer alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza nadharia ya upitishaji umeme. Mwaka wa 1972, pamoja na John Bardeen na Leon Cooper alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

Melvin Schwartz

Melvin Schwartz alikuwa mwanafizikia Mwamerika. Mwaka 1988 alipokea Tuzo ya Nobel ya Fizikia pamoja na Leon Max Lederman na Jack Steinberger kwa mafanikio yao ya kugundua mbinu za kushughulika maneutrino ambazo ni chembe ndogo sana ya kinyuklia i ...

                                               

Julian Schwinger

Julian Schwinger alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza nguvu za umeme na nadharia ya kwanta. Mwaka wa 1965, pamoja na Richard Feynman na Shinichiro Tomonaga alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

Glenn Seaborg

Glenn Theodore Seaborg alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza elementi nzito sana. Mwaka wa 1951, pamoja na Edwin McMillan alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Emilio Segre

Emilio Segre alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Italia. Mwaka wa 1938 alihamia Marekani. Hasa alifanya utafiti wa fizikia ya kiini. 1937 alitambua Tekineti kama elementi sintetiki ya kwanza iliyopatikana katika historia. Mwaka wa 1959, pamoja na ...

                                               

Nikolay Semyonov

Nikolay Nikolayevich Semyonov alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Urusi. Hasa alichunguza nishati mwendo. Mwaka wa 1956, pamoja na Cyril Hinshelwood alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Shibasaburo Kitasato

Shibasaburo Kitasato alikuwa mtoto wa kwanza wa aliyekuwa Meya wa kijiji kidogo huko nchini Japan. Alisoma kuhusu dawa katika chuo kikuu cha Tokyo na kumaliza mwaka 1883 baada ya kufanya kazi katika ofisi ya afya ya umma. Alitumia miaka sita nchi ...

                                               

William Shockley

William Bradford Shockley alikuwa mhandisi na mwalimu kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza mambo ya umeme na kuvumbua transista. Mwaka wa 1956, pamoja na John Bardeen na Walter Brattain alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

Kai Siegbahn

Kai Manne Börje Siegbahn alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uswidi. Alikuwa mtoto wa Karl Manne Siegbahn. Hasa alichunguza mnururisho wa kiini cha atomu. Mwaka wa 1981, pamoja na Nicolaas Bloembergen na Arthur Schawlow alikuwa mshindi wa Tuzo ya ...

                                               

Karl Manne Georg Siegbahn

Karl Manne Georg Siegbahn alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uswidi. Alichunguza vipengele vingi vya fizikia, baadhi yao usumaku, mionzi ya eksirei na nadharia ya atomu. Mwaka wa 1924 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Mwana wake ni mw ...

                                               

Frederick Soddy

Frederick Soddy alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alichunguza unururifu. Aliunda istilahi mpya ya isotopu. Mwaka wa 1921 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Wendell Stanley

Wendell Meredith Stanley alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza kugandisha virusi kama fuwele. Mwaka wa 1946, pamoja na James Sumner na John Howard Northrop alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Johannes Stark

Johannes Stark alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza maswali ya umeme. Mwaka wa 1905 aligundua athari ya Doppler katika mionzi maalumu. Mwaka wa 1919 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

Hermann Staudinger

Hermann Staudinger alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza plastiki laini. Mwaka wa 1953 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

William Stein

William Howard Stein alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza mifumo na athari za protini. Mwaka wa 1972, pamoja na Christian Anfinsen na Stanford Moore alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Jack Steinberger

Jack Steinberger alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Alizaliwa Ujerumani lakini akapahama wakati wa utoto wake kwa sababu ya utawala wa Wanazi. Hasa alichunguza sehemu za atomu na kujulikana kwa kugundua neutrino ya muon. Mwaka wa 1988, ...

                                               

Lord Rayleigh

Lord Rayleigh alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa John William Strutt. Baadhi ya utafiti mwingine aligundua elementi ya agoni. Mwaka wa 1904 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

James Sumner

James Batcheller Sumner alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza vimengenya. Mwaka wa 1946, pamoja na John Howard Northrop na Wendell Stanley alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Theodor Svedberg

Theodor Svedberg alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Sweden. Baadhi ya uchunguzi mwingi aliunda aina ya mashinepewa. Pia alitafiti mada za fizikia ya kiini. Mwaka wa 1926 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Svyatoslav Fyodorov

Svyatoslav Nikolayevich Fyodorov alikuwa mtaalamu wa macho wa Urusi, mwanasiasa, profesa, mwanachama kamili wa Chuo cha Urusi cha Sayansi na Chuo cha Urusi cha Sayansi ya Tiba. Anachukuliwa kuwa mwanzilishi wa upasuaji wa kurekebisha kasoro za macho.

                                               

R.L.M. Synge

Richard Lawrence Millington Synge alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alichunguza mbinu za kutenganisha dutu zinazofanana. Mwaka wa 1952, pamoja na Archer John Porter Martin alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Igor Tamm

Igor Yevgenyevich Tamm alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Urusi. Hasa alichunguza uhusiano kati ya elektroni na nuru. Mwaka wa 1958, pamoja na Pavel Cherenkov na Ilya Frank alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

Theodor Curtius

Geheimrat Julius Theodor Curtius alikuwa profesa wa Kemia wa Ujerumani katika Chuo Kikuu cha Heidelberg. Yeye ndiye aliyegundua kampaundi nyingi za diazo, hydrazini na asidi hidrazoiki. Alisoma kemia na mwenzie Robert Bunsen katika Chuo Kikuu cha ...

                                               

Thomas Robert Malthus

Mch. Thomas Robert Malthus FRS alikuwa mchungaji wa Kianglikana na mtaalamu wa uchumi aliyetunga nadharia maarufu kuhusu demografia, hasa uhusiano kati ya ongezeko la watu na kiasi cha bidhaa zinazopatikana.

                                               

George Thomson

George Paget Thomson alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alichunguza elektroni. Mwaka wa 1937, pamoja na Clinton Davisson alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Thomson ni mwana wa Joseph John Thomson aliyetuzwa Tuzo ya Nobe ...

                                               

Joseph John Thomson

Joseph John Thomson alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa anajulikana kwa kugundua elektroni. Mwaka wa 1906 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Mwaka wa 1908 alipewa cheo cha Sir cha Uingereza. Pamoja na gunduzi zake muhimu ...

                                               

Samuel Ting

Samuel Chad Chung Ting alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uchina. Alipokuwa na umri wa miaka 20 alihamia Marekani. Hasa alichunguza nadharia ya atomu. Mwaka wa 1976, pamoja na Burton Richter alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

Arne Tiselius

Arne Wilhelm Kaurin Tiselius alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uswidi. Hasa alichunguza mbinu za kutenganisha protini. Mwaka wa 1948 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Alexander Todd

Alexander Robertus Todd of Trumpington alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alichunguza mfumo wa nukleotidi na usanisi wake. Mwaka wa 1957 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Shinichiro Tomonaga

Shinichiro Tomonaga alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Japani. Hasa alichunguza nguvu za umeme na nadharia ya kwanta. Mwaka wa 1965, pamoja na Richard Feynman na Julian Schwinger alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

Charles Townes

Charles Hard Townes alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza mionzi ya aina mbalimbali na kuvumbua leza. Mwaka wa 1964, pamoja na Nikolai Basov na Aleksander Prokhorov alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

John Van Vleck

John Hasbrouck Van Vleck alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza nadharia ya atomu, na usumaku. Mwaka wa 1977, pamoja na Philip Anderson na Nevill Mott alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

Artturi Ilmari Virtanen

Artturi Ilmari Virtanen alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Finland. Baadhi ya utafiti mwingi alichunguza virusi vikaavyo kwenye udongo. Mwaka wa 1945 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Vladimir Belousov

Vladimir Vladimirovich Belousov alikuwa mwanasayansi wa Dunia katika Umoja wa Kisovyeti, na mwanasheria maarufu wa njia mbadala za nadharia za Umoja wa Kisovyeti. Beloussov alikuwa mkuu wa Idara ya Geodynamics ya taasisi ya Fizikia ya Dunia huko ...

                                               

Otto Wallach

Otto Wallach alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza michanganyiko kama terpini. Mwaka wa 1910 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Ernest Walton

Ernest Walton alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ireland. Hasa alichunguza mwendo wa vijipande vya atomu. Mwaka wa 1951, pamoja na John Douglas Cockcroft alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

Steven Weinberg

Steven Weinberg alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza usumaku. Mwaka wa 1979, pamoja na Sheldon Glashow na Abdus Salam alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

Alfred Werner

Alfred Werner alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uswisi. Pamoja na utafiti mwingine alichunguza elementi ya naitrojeni. Mwaka wa 1913 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Heinrich Otto Wieland

Heinrich Otto Wieland alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Alihariri kumbukumbu za kikemia za Justus von Liebig. Pia alichunguza mifumo ya kikemia ya sumu za uyoga na asidi ya nyongo. Mwaka wa 1927 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

                                               

Wilhelm Wien

Wilhelm Wien alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza mambo ya mnururisho. Mwaka wa 1911 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

                                               

Eugene Wigner

Eugene Paul Wigner alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Alizaliwa nchi wa Hungaria na jina Jenó Pál Wigner. Hasa alichunguza nadharia ya atomu. Mwaka wa 1963, pamoja na Johannes Hans Daniel Jensen na Maria Goeppert-Mayer alikuwa mshindi ...

                                               

Geoffrey Wilkinson

Geoffrey Wilkinson alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alichunguza metali. Mwaka wa 1973, pamoja na Ernst Otto Fischer alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia. Mwaka wa 1976 alipewa cheo cha "Sir".